MCT yatangaza majina ya wateule wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

EJAT (2)

MCT yatangaza majina ya wateule wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2015 Kamati ya maandalizi ya EJAT 2015 imetangaza majina 84 ya wateule wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2015. Idadi hiyo ni ongezeko la wateule 31 ukilinganisha na tuzo za 2014 ambapo wateule walikuwa ni 53 tu.

Pia kamati imeeleza kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tom Bahame Nyanduga ndio Mgeni Rasmi kwenye Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT ) 2015 zitakazofanyika kwenye tamasha la usiku la utoaji wa tuzo hizo Aprili 29, 2016 , Dar es Salaam.

Kutangazwa kwa wateule wa EJAT 2015 kunafuatia kukamilika kwa kazi ya kuzipitia na kuchagua zile zilizo na ubora zaidi iliyofanywa na jopo la majaji 10 lililokaa mwezi Machi mwaka huu. Majaji hao ambao ni wataalamu mbalimbali wa masuala ya habari walipitia kazi za kiandishi zaidi ya 570 zilizowasilishwa kwenye makundi ya kushindaniwa 22 kwenye tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2015.

Kilimanjaro Film Insitute inaongoza kwa kutoa washiriki wengi kwa upande wa TV(Runinga) ambapo imetoa washiriki nane ambao wanashiriki kinyang’anyiro hiki. Usikose kufuatilia Tuzo hizi ifikapo mwisho wa juma hili. 29 April 2016 kuanzia saambili usiku.